Utangulizi
SHADE pre and primary school ipo katika kata ya ibadakuli mkoani wa shinyanga. Shule ipo umbali wa KM 7 kutoka Manispaa ya Shinyanga. Shule ilianzishwa na kusajiliwa mnamo tarehe 19/11/2021 kwa namba za usajili EM 18928. Shule ni ya kutwa na ni moja ya miradi inayoendeshwa na shirika la SHADE lililopo mkoani Shinyanga. Taassisi ina maono thabiti ya kuwawezesha wanafunzi kufikia ubora wa kitaaluma na kuondoa changamoto za kiakili na kimwili na kuwafanya watoto wawe viongozi bora wa baadaye ili waweze kubadirisha dunia katika mtazamo chanya. Tunaamini watoto wakipata msingi bora watakuwa wawajibikaji katika jamii na hivyo kuwa na Taifa lenye nguvu.
Kwa bidii yetu yote tumeifanya kuwa dhamira yetu:
- Kutoa elimu bora na jumuishi ambayo ni chimbuko la ukuaji wa kiakili, kiroho na kimwili. Kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi sahihi kutokana na mzingira, kuwasaidia na kukidhi mahitaji yao yote muhimu wawapo shuleni.
- Kukuza fikra zao pamoja bila kujali tofauti za mwanafunzi kwa kuwafanya wawe viongozi bora wa baadae ili waweze kubadirisha dunia.
- Kuanzisha mfuko wa ufadhili wa elimu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ili wapate elimu bora bure.
Hivyo basi maono haya tumeyakumbatia na kuweka nguvu kwa kila mfanyakazi wa Shule na shirika kutimiza maono haya kwa wanafunzi wetu, Shule itapata mafanikio makubwa sana kwa miaka mingi ijayo, ni dhamira yetu kuifanya SHADE kuwa uwanja wa kupumzika kwa watoto wenye mazingira magumu, kulea viongozi wa Tanzania na Kimataifa.
Kauli Mbiu
Kukuza viongozi, kubadirisha dunia
Mawasiliano
Simu: +255763543456, +255744087584
Tovuti: www.shadetz.org
Barua pepe: school@shadetz.org
Ada za Shule
Ada zetu ni nafuu sana kwani tumezingatia ubora zaidi, kwa mwaka 2024 Shule ya SHADE ina madarasa sita yaani (awali) madarasa matatu na (msingi) madarasa matatu (darasa la kwanza, la pili na darasa la tatu).
Awali
- Ada ya awali ni 700,000 kwa mwaka.
- Usafiri ni 400,000 kwa mwaka. Jumla ya Ada na Usafiri ni 1,100,000 kwa mwaka.
- Ada hii hulipwa mara nne kwa mwaka, kila baada ya miezi 3.
Jan – Mar | Apr – Jun | Jul – Sep | Oct – Dec |
275,000 | 275,000 | 275,000 | 275,000 |
Msingi
- Ada ya Elimu ya msingi ni 900,000 kwa mwaka.
- Usafiri ni 400,000 kwa mwaka. Jumla ya Ada na Usafiri ni 1,300,000 kwa mwaka.
- Ada hii hulipwa mara NNE kwa mwaka.
Jan – Mar | Apr – Jun | Jul – Sep | Oct – Dec |
325,000 | 325,000 | 325,000 | 325,000 |
Mfuko wa ufadhili wa elimu kwa watoto wenye mazingira magumu
Shule ya SHADE inatoa fursa nzuri ya mfuko wa ufadhili wa elimu kama kipaumbele kwa watoto wenye ualbino na wenye mazingira magumu na hatarishi katika manispaa ya Shinyanga, watoto hawa hupata elimu bora na bure kabisa kuanzia darasa la 1 hadi darasa la 6.
Tunaamini katika elimu jumuishi hivyo SHADE haikuwaacha watoto wengine wanaoishi katika mazingiira magumu mfano yatima, wanaoishi na mzazi mmoja, pia hawa watoto wanapata elimu bora na bure hadi watakapo maliza darasa la 6.
Maneno ya kujenga misingi kwa watoto
Ubora, Nidhamu na Upendo